top of page
C-Sema Team

Mambo ya kufanya kabla ya kupata ujauzito

Unaweza kuwa hujapata ujauzito bado lakini kuna mengi unaweza kufanya ili kuhakikisha afya njema kwako na mtoto atakayekuwa tumboni mwako. Ifanye hii kuwa orodha yako binafsi yenye vitu uakavyohitajika kushughulikia.



Weka miadi na daktari wako / kliniki yako. Ukweli ni kwamba utakutana naye mara nyingi mara baada ya kuwa mjamzito. Hivyo ni vyema ukaweka miadi mapema kabla hujamtembela hata kama ulishawahi kuwa mjamzito hapo kabla. Kama una tatizo lolote la kitabibu linaloweza kuathiri uwezo wako wa kupata ujaizito au kuuweka ujauzito wako katika hatari ni bora utafutie matatizo hayo ufumbuzi sasa.

Kama kwenye familia yako kuna ugonjwa wa ugonjwa wa seli nundu (sickle cell disease) ama ugonjwa mwingine wowote wa kurithi unaweza tafuta msaada toka kwa mtaalamu wa kijenetiki au kufanya vipimo vya kutathimini kama una magonjwa kama hayo au mengine yanayoweza kuathiri kupata ujauzito au kuathiri mimba kabla ya kupata ujauzito.

Chunguza afya ya fizi zako. Kuna uhusiano wa karibu kati ya kinywa chenye afya na ujauzito wenye afya. Magonjwa ya fizi yanaweza kuwa ishara ya kuwa kwenye hatari ya kujifungua kabla ya wakati au kupata mtoto njiti. Hivyo huu ndiyo wakati muafaka kumwona daktari wa afya ya kinywa na meno ili ashughulikie tatizo lako lolote la kinywa.

Sitisha uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe. Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe katika kipindi cha ujauzito siyo salama. Vitu hivi siyo vizuri kwa mtoto tumboni na vinaweza kumuathiri hata baada ya kuzaliwa.

Pamoja na hayo yote uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe unaweza kukusabishia iwe ngumu kupata ujauzito au kuongeza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu. Ongea na daktari wako kuhusu mpango wa wewe kuacha vitu hivyo.

Sitisha matumizi ya vidonge vya uzazi wa majira ili kupata ujauzito. Je, ni muda kiasi gani unahitajika kwa dawa na vidonge vya uzazi wa mpango kuisha mwilini? Inawezekana kupata ujauzito mara tu baada ya kuacha kutumia dawa za uzazi wa mpango. Mara baada ya vichocheo vya dawa kuwa vimekwisha kwenye mwili ingawaje kiuhalisia inaweza kuchukua mpaka miezi kadhaa kabla upevushaji wa mayai haujaanza kama ilivyokuwa hapo awali. Je, ni salama kupata ujauzito punde tu baada ya kuacha matumizi ya vionge vya dawa za uzazi wa mpango? Ndiyo ni salama kupata ujauzito mara tu baada ya kuacha matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.


Punguza matumizi ya kafeni. Kunywa vikombe viwili vya kahawa au soda tano kwa siku amabzo ni sawa na miligramu 250 za kafeni kunaweza kufanya iwe vigumu kwako kupata ujauzito na pia kuongeza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu.

Kuacha matumizi ya kafeni kuna faidia nyingine zaidi. Utajiepusha na uraibu unaotokana na matumzi ya kafeni kapindi cha wiki za kwanza za ujazito.


Zingatia lishe bora katika ulaji wako. Huu ni wakati wa kusitisha vyakula vya viwandani na vyenye lishe hafifu. Hakikisha unapata matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka kamili (unga usiokobolewa, n.k.) na protini kiasi kila siku.

Lishe bora inaweza kukupunguzia hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari uanotokea wakati wa ujauzito unaoathiri akina mama wajawazito.


Punguza uzito wa ziada. Uzito wa ziada unaweza kukuongezea hatari ya kupata kisuakari cha mimba na mara nyingine shinikizo la damu linalotokea wakati wa ujauzito na ambalo linaloweza kupelekea kupata kifafa cha mimba.

Haishauriwi kujaribu kupunguza uzito ukiwa mjamzito, hivyo kama unataka kupunguza uzito wako anza mapema kabla hujashika ujauzito.


Changamkia chanjo. Baadhi ya magonjwa katika kipindi cha ujauzito yanayweza kukuweka taabani. Yanaweza kuleta madhara kwa mwanao. Ongea na daktari kuhusu chanzo zipi utazihitaji sasa na zipi utakazohitaji baadae.


Katika nchi yetu ya Tanzania, akina mama wajawazito hupata chanjo dhidi ya pepopunda (tetanasi) mapema iwezekanavyo katika ujauzito. Anatakiwa kupewa chanjo nyingine wiki 4 baadaye iwapo atakuwa hajapata chanjo zote. Hii husaidia kuwalinda wote wawili-mama na mtoto wake.


Tafakari kuhusu dawa unazotumia. Ni muhimu kumjulisha daktari wako kuhusu dawa zote unazotumia. Kutumia dawa dawa hasa zile unazonunua bila kuandikiwa na daktari ikiwa ni pamoja na dawa miti shamba (za kienyeji) na vitamini kunaweza kuwa hatari kwako na kwa mwanao.


Huu pia ni wakati wako kutumia vitamini au vidonge vya foliki ili kupunguza uwezekano wa kupata mtoto mwenye dosari za kimaumbile. Dawa zote zitumike kwa ushauri wa daktarin na si vinginevyo.


Chagua samaki wa kula. Samaki wanao uwezekano mkubwa wa kuwa na sumu nyingi kama zibaki (mercury) zinazotokana na uvuvi haramu wa kutumia mabomu au sumu. Kumbuka inaweza kukuchukua karibia mwaka mmoja hadi sumu zote kuwa zimekwisha mwilini mwako.

Hivyo punguza ulaji wa samaki hadi walau mara mbili kwa wiki. Ikiwezekana epuka kabisa ulaji wa samaki wafuatao wenye uwezekano wa kuwa na kiwango kikubwa cha zebaki, ambao ni papa, chuchunge na nguru.


Fanya mazoezi. Sio tu kwamba mazoezi yatakuweka katika uzito mzuri lakini pia mazoezi yatakuandaa kwa ajili ya uchungu na kujifungua. Unapokuwa mjamzito tafuta namna ya kufanya mazoezi na ukiweza kupata sehemu yalipo mazoezi kwa ajili ya wajawazito itapendeza sana.


Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org


1 view
bottom of page