top of page
  • C-Sema Team

Mambo 7 usiyoyafahamu kuhusu mahakama ya watoto.


Je ukiwa kama mzazi ama mlezi unafahamu nini juu ya mahakama ya watoto?

Mara nyingi haki hupotea kwa kutozijua sheria na namna vyombo mbalimbali vya utoaji haki vinavyo endeshwa. Mahakama ni chombo maalumu katika utoaji wa haki na kuhakikisha haki inatendeka. Kuna aina nyingi za mahakama Tanzania Bara na Visiwani ikiwemo Mahakama ya Rufaa, Mhakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Mwanzo zote hizi husikiliza mashauri ya makosa ya jinai na madai. Lakini leo tutazungumzia mahakama maalumu ambayo ni mahakama ya watoto.


Ilianza rasmi mwaka 2009. Mahakama hii kisheria ilianzishwa ili kulinda haki za mtoto na kusikiliza mashauri yote yanahusuyo mtoto wa kitanzani. Sheria ya mtoto namba 21 ya Mwaka 2009 inafafanua kuwa mtoto ni mtu yoyote aliye chini ya miaka 18. Ambapo sheria hii ndio iliyoanzisha mahakama hii ya watoto. Japo mahakama huwa na jukumu la kuhakikisha haki inapatikana na adhabu stahiki inatolewa zifuatazo ni kazi za Mahakama ya watoto Tanzania. Mashauri ya mahakama ya mtoto mara nyingi huendeshwa na Hakimu Mkazi.


Mahakama ya watoto husikiliza na kuamua mashauri ya jinai dhidi ya mtoto. Makosa ya jinai kwa watoto huweza kufanyika kokote mfano shuleni, mtaani, nyumbani hata makanisani. Hutokea katika mazingira ya kila siku yam toto. Ili kumpatia haki stahiki mtoto huyu mashitaka yake huweza sikilizwa katika mahakama ya watoto tofauti na makossa yafanywayo na mtu Zaidi ya miaka 18. Na mara nyingi mashauri haya hufanywwa faragha ili kulinda maslahi ya mtoto.


Haki ya mzazi / mlezi kuwepo mahakamani. Wakati mashauri haya yanaendelea ni haki na wajibu wa mzazi ama mlezi au ofisa ustawi wa jamii kuwepo. Hii ni muhimu ili kumfanya mtoto kujihisi salama na kuhakikisha mhakama inatenda haki. Pia katika utoaji wa ushahidi watoto wengi hujihisi faraja na kuwa na uhuru wa kutoa ushahidi tofauti na pale ambapo uwepo wa mzazi ama mlezi unakosekana. Afisa ustawi wa jamii mara nyingi huwepo mahakamani kuhakikisha maslahi ya mtoto anayeshtakiwa / ama kutoa ushahidi yanazingatiwa.

Kuwakilishwa na wakili. Ni muhimu kwa mzazi kujua kwamba mtoto anayeshtakiwa ana haki ya kuwa na ndugu wa karibu au kuwakilishwa na wakili katika mashauri yote. Hii ni muhimu hasa pale ambapo mtoto atahitaji kukatiwa rufaa na kama haki hii ipo hakimu hana budi kuifafanua wazi wazi ili ieleweke kwa mtoto, ndugu ama wakili wake.


Uhuru wa maoni na kusikilizwa kwa maoni yake. Fahamu kuwa mtoto huyu amehakikishiwa haki yake ya kutoa maoni ama ufafanuzi wa namna yoyote bila kupewa kipingamizi na mahakama hii. Haki hii ni ya kikatiba kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 13 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaongelea usawa na haki ya kusikilizwa kwa kila mtanzania.


Maamuzi kufikiwa ndani ya siku moja tu. Mara nyingi mashauri yote tofauti na mashauri ya kosa la mauaji husikilizwa ndani ya siku moja tu na ndani ya siku hiyo hiyo hukumu hutolewa yote hii ni kuzingatia maslahi ya mtoto na kuepuka kumchosha na taratibu za kuahirishwa kwa kesi.


Utaratibu wa mahakam hii mara nyingi siyo rasmi. Pamoja na kwamba mahakama hii huwa na mazingira rafiki kwa mtoto vilevile huendesha mashauri yake kwa lugha ya Kiswahili ama Kiingereza kama lugha rasmi. Lakini iwapo mtoto atashidwa kusoma kwa lugha ya Kiwahili ama Kiingereza ni wajibu wa mahakama kumpatia mkalimani. Na kama atahitajika kusaini kokote inabidi asomewe, afafanuliwe na apewe nafasi ya kumshirikisha mzazi ama muwakilishi wake katika zoezi zima la utiaji wa saini. Ni muhimu kwa wazazi kuzingatia haya ili kuhakikisha haki ya mtoto haipotei na maslahi yake yanazingatiwa.


Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org


photo credit: @MwananchiNews

0 views

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page