top of page
C-Sema Team

Kuzaliwa hadi mwaka wa kwanza wa maendeleo ya mwanao.

Kumhumdumia mtoto mdogo (chini ya mwaka mmoja) linaweza kuwa jambo la kuchosha lakini kuna mengi ya kutumainia. Chukua muda wako kutembea pamoja nasi katika kuangalia safari ya mwanao toka kuzaliwa mpaka kufikisha mwaka mmoja.



Tababsamu.

Baada ya miezi miwili ya kukesha kwa kubembeleza huku ukishuhudia mengi ya machozi ya mwanao na wakati wote huo ukitarajia kwa hamu kuona angalau tababsamu kwake bila matumaini. Sasa ni wakati wako wa kufurahia tababsamu la mwanao. Kuanzia miezi 2 na kuendelea mwanao anaweza kuwa anatabasamu sasa. Kila unapomchekea au kumtekenya au hata kumwangalia kwa tabasamu naye atakuangalia kwa tabasamu.


Kicheko.

Endapo sauti ya mwanzo ya mwanao hukuwa unaielewa, sasa kufikia mwezi wa nne mwanao anaanza kutoa sauti nzuri ya kitoto. Pengine ni sauti tamu ambyo haitoki kwa mwingine bali ni kwa mwanao mwenyewe akicheka pamoja na wewe. Tumia wakati huu kumchekea na kumchekesha. Inapendeza sana.


Kulala usiku kuchele.

Sawa kabisa. Hili ni jambo ambalo linaweza kuonekana haliwezekani kwa wazazi wachanga waliohangaika kuamka mara kwa mara usiku kwa ajili ya kumbembeleza mtoto anayelia. Usihofu kwani kufikia mwezi wa 4 mpaka 6 mtoto anaweza kuanza kulala usingizi usiku kucha kama hana shida yeyote inayohitaji msaada wa kitabibu. Wapo baadhi ya watoto ambao bado watahitaji kuamka – haina maana ni wagonjwa. Bado ni jambo la kawaida.


Kukaa.

Kuanzia miezi 4 mtoto huwa ameanza kukaza shingo na kuanzia miezi 5 mpaka 6 mtoto huwa ameanza kukaa ila kwa kushikiliwa huku mikono ikiwa imeelekea mbele au ikiwa imeshikilia kitu fulani mathalani kiti n.k.. Mtoto anaweza kuketi bila kushikilia au kushikiliwa kuanzia miezi 7 mpaka 9.


Kutambaa.

Kutambaa siyo hatua ya lazima kwa baadhi ya watoto kwani wengine huruka na kuanza kutembea. Hata hivyo katika kipindi hiki mwanao huwa ameanza kutambaa na kuzunguka nyumba weka vitu vyako vya hatari kwa mtoto mbali na maeneo anayoyafikia. Kufikia miezi 9 watoto wengi huwa wanatamabaa kwa kutumia mikono yao na miguu pia.


Kupunga mkono wa kwa-heri (bai bai - bye -bye).

Kufikia miezi 9 watoto wengi huwa wameanza kuelewa na kuunganisha kati ya ishara, sauti na maana zake. Kumbuka kupunga mkono siyo tu kwamba ni tendo zuri lakini pia kitendo cha kung'amua na kutumia lugha za ishara. Wanatambua kwamba kupunga mkono kuna mahusiano na neno kwa-heri.


Kula chochote wanachokiona.

Kuanzia miezi 9 mpaka 12 watoto wanauweza kudhibiti miili yao na wanaweza kutumia mikono na miguu yao. Katika kipindi hiki huwa wanapenda kukamata na kula chochote kile kilicho mbele yao. Hii ni kwa sababu wanajaribu kuichunguza na kuigundua milango yao ya fahamu ya ladha na mguso. Hiki ndicho kipindi ambacho wazazi huwa wahangaika katika kuwadhibiti watoto wao wasile uchafu au vitu visivyofaa.


Kusimama.

Kufikia miezi 12 watoto wengi huwa wameweza kusimama bila ya kuegemea. Wanaweza kuanza kutembea hatua ndogo huku wakiwa wameegema au kushiklia kitu fulani. Kuanzia miezi 13 au zaidi wengi wao huwa wanaweza kutembea bila ya kushilika kitu. Wiki chache baadae huwa wanaweza kutembea.


Kupiga hatua ya kwanza.

Pengine panaweza pasiwepo hatua nyingine muhimu katika maendeleo ya mtoto kuliko yeye kuanza kupiga hatua ya kwanza peke yake. Kipndi cha kawaida cha watoto kuanza kutembea mara nyingi huwa ni kuanzia miezi 9 mpaka 17.


Kuanza kuongea neno la kwanza

Ukitaka kujua umuhimu wa kuanza kuongea kwa mtoto mtafute mzazi ambaye mwanae amechelewa kuongea na piga picha furaha yake itakuaje pale ambapo mwane atakapotmaka neno la kwanza. Kuanza kuongea kwa mtoto mara nyingi huanza baada ya mtoto kufika mwaka mmoja ingawa baadhi ya watoto wanaweza wakatamka neno la kwanza mapema kidogo. Baada ya hapa haitachukua muda mrefu kabla ya mwanao kuanza kuongea. Kama mwanao utaona anachelewa kuongea mwone daktarin wa watoto.


Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org

Picha ni kwa hisani ya gazeti la Mwananchi.

1 view
bottom of page