Mkurugenzi wa kituo cha kushughulikia matatizo ya usingizi kwa watoto kilichopo hospitali ya Bostoni Daktari Richard Feber amefanya tafiti na kuvumbua njia inayojulikana kama ‘uangalizi endelevu’ ambayo lengo lake ni kumsaidia mwanao kupata usingizi mwenyewe bila kutegemea kubembelelezwa au kuhamasishwa hata pale atakapoamka aweze kulala tena mwenyewe.
Hata hivyo daktari huyo anashauri mbinu hii ianza kutumike angalau mtoto anapokuwa ana umri wa miezi 5 mpaka 6. Hizi hapa ni hatua za kuafuata katika kumsaidia mwanao kupata usingizi kwa kutumia njia ya ‘uangalizi endelevu.’
Muweke mwanao kitandani mara tu anapoanza kusinzia lakini bado hajalala kabisa. Baada ya kumaliza maandalizi ya hapo kitandani toka na muache kitandani akiwa bado hajasinzia.
Hata kama mwanao atalia subiri kwa dakika chache kabla kwenda kumwangalia tena. Muda utakaosubiri unategemea mazoea yako wewe na mwanao. Unaweza kusubiri 1 mpaka 5 au zaidi.
Baada ya muda wa dakika zako kutimu ingia chumbani alipolala na jaribu kumbembeleza lakini usimbebe wala usikae zaidi ya dakika 2 au 3 kisha ondoka hata kama bado analia. Hii ni kwa sababu kuona uso wako pekee kutamhakikishia kwamba bado upo karibu naye na hivyo anaweza kuendelea kulala yeye mwenyewe.
Kama ataendelea kulia, ongeza muda wa kusubiri kabla ya kwenda kumuona. Mathalani kama ulikuwa ukichukua dakika 5 kabla ya kwenda kumuona tena basi sasa ongeza mpaka dakika 7. Akiendelea sasa utakapoenda tena ongeza mpaka dakika 10 endapo bado atakuwa analia.
Usiku unaofuata ongeza kuanzia dakika 5 mara ya kwanza, kisha dakika 10 na baadae dakika 12, n.k.
Ili kuzoea mbinu hii itakuchukuwa muda lakini usichoke wazazi wengi huaanza kuona mabadiliko kuanzia siku ya 3 au ya 4. Wengine huona mabadiliko hata zaidi ya wiki moja.
Dokezo: Hakikisha unapata usingizi wa kutoshs usiku mmoja kabla ya kuanza mafunzo haya ya ‘uangalizi endelevu’ kwa mwanao. Kwani katika siku ya kwanza utatumia muda mwingi kusikiliza mwanao akilia, kuangalia saa, kuingia kumwangalia na kisha kutoka. Hivyo utahitaji nguvu na umakini ambao hauwezi kuupata uwapo na usingizi.
Elewa kwamba itahitaji moyo kumsikia mwanao akilia pasi wewe kuwiwa kumpakata na kumbembeleza. Wazazi wengi wameshindwa kufikia malengo kwa sababu ya kutoweza kuvumila na kuwaacha watoto wao kulia pekee yao. Hata hivyo mvumilivu hula mbivu. Ijaribu.
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzani
Kommentare