top of page
  • C-Sema Team

Zijue mbivu na mbichi kuhusu kumlisha mwano kwa kutumia chupa


Kuhusu glasi au chupa ya kulishia.

Kuna chupa za aina mbili zinazotumika katika kulishia mtoto maziwa. Chupa za glasi au chupa za plastiki. Ingawa zipo chupa nyingi za plastiki, unapochagua chupa jitahidi kujiridhisha kuwa hazina kemikali ya bisphenol inayotumiwa kama moja ya viambata vya kutengeneza chupa za plastiki. Zipo chupa nyingi za plastiki zisizo na kemikali hiyo ya bisphenol.


Kuhusu chuchu za chupa.

Chuchu za chupa za kunyonyeshea zinatofautiana kunzia malighafi au viambata vilivyotumika kuitengeneza mathalani latex au silicone, mpka ukubwa wa ujazo wa chupa na matobo ya chuchu. Ukubwa wa tobo huathiri kiwango cha maziwa kinachotoka kwa wakati husika. Hivyo unaweza kujaribu kuona mwanao anapenda chupa gani na yenye chuchu gani. Pamoja na kuangalia ubora wa chupa inayotumika kumbuka kuangalia kama chupa zako ni nzima hazijapasuka au hazina michubuko. Kila mara badili chupa zilizo na hitilafu kulinda afya ya mtoto wako.


Jinsi ya kuosha chupa zako.

Osha chupa kila mara baada ya kutumika kwani zinaweza kuwa chanzo cha maambukizi kwa mwanao. Zioshe kwa maji ya moto na sabuni. Unapokuwa unziosha usisahsu kuangalia chuchu zako kama ni nzima au zimepasuka, kuchubuka, n.k.


Maziwa maziwa ya kopo yenye kanuni za unyonyeshaji.

Unapokuwa unampatia mwanao maziwa ya chupa, yawe uliyokamua au ya kopo yenye kanuni za unyonyeshaji usiyaongeze maji kinyume na maelekezo. Unapotumia maziwa ya kopo changanya kulingana na maelekezo kwenye karatasi ya mtengenzaji kwani kuweka maji mengi unaharibu kanuni na kuvifanya virutubisho kupungua, mathalani utafanya kiwango cha chumvi kupungua kitendo ambacho kinaweza kumfanya mtoto akapata degedege na kiwango kidogo cha maji kinaweza kuwa na madhara kwa figo na hata tumbo la mwanao.


Nitajuaje maziwa haya yanafaa kwa mwanangu?

Yapo maziwa ya aina nyingi kutoka kwenye soya na yale ya ng'ombe. Wazazi wengi hupendelea maziwa ya ng'ombe ingawa huwa yameambatana na mzio (allergy). Unaweza kutumia maziwa ya soya kwani huwa hayana mzio. Unaweza kutumia maziwa ya unga yaliyokolezwa au yaliyo tayari kwa kutumika. Kumbuka kununua maziwa yaliyoongezewa madini ya chuma.


Je, joto la kwenye maziwa yako linahusu?

Tikisa maziwa yako kabla ya kumpatia mwanao. Ni vyema ukampatia manao maziwa ya ya uvuguvu ya joto la kawaida. Kama anapendelea maziwa ya joto la kawaida mpe hayo hayo, na kama ni ya uvuguvugu mpe hayo pia. Usichemshe maziwa yako kwenye mikrowave kwani katika kuchemsha maziwa yako unaweza kuua kingamwili zilizomo kwenye maziwa.


Usiache kumshikilizia mwanao chupa wakati wa kunyonya.

Unapokuwa ukimpatia mwanao maziwa ya chupa usimuache akajishikia chupa na kunywa mwenyewe kwani anaweza kupaliwa au kupatwa na maambukizi ya sikio. Kumshikia chupa mtoto wakati wa kunyonya humsaidia mama / baba kuimarisha upendo kati mtoto na mama / baba.


Kujua kama mwanao ameshiba?

Pale mwanao anapokuwa ameshiba anaweza kuacha na kutema maziwa, kugeukia upande mwingine, atasukumia mbali ziwa au chupa ya maziwa. Huna haja ya kumlazimisha kuendelea kunyonya. Hata hivyo unaweza kujaribu kumpa baadaye kama bado hataki basi jua ameshiba.


Jinsi ya kumfanya mwanao kubeua.

Baadhi ya watoto hutapika kila wanapokuwa wanayonya au wanapomaliza kunyonya. Kuwalaza begani au kuwalaza kwenye mapaja yako wakiwa wamelalia tumbo lao na kuwapigapiga mgongoni kunaweza kuwasaidia sana. Wakati ukifanya hivyo anaweza kubeua / kucheua baadhi ya maziwa na usiwe na wasiwasi mfute maziwa hayo kwa kitambaa na hata kama hajabeua uiswe na wasiwasi pia kwani sio kila mtoto anabeua.


Punguza kutema maziwa kwa mwanao.

Kama mwanao anatema maziwa sana au anabeua sana anapomaliza sana kunyonya, chelewesha kucheza naye mpaka baada ya dakika 45 baada ya kula. Mpigepige kila baada ya dakika chache wakati anapokuwa anakula ila si wakati wa kumeza. Kutema au kubeua hunapungua pale mtoto anapokuwa amekaa wima. Kama unaona kwamba bado anabeua sana muone daktari.


Je, upi wakati muafaka wa kubadilisha maziwa anyotumia mtoto?

Kabla ya kufikri kubadili aina ya maziwa ya kanuni (formula) unayotumia ni vizuri ukawasiliana na daktari akakushauri nini cha kufanya. Hata hivyo kumbuka kuwa mtoto anaweza kukataa maziwa kila unapompa na hii inaweza kuwa shida ya aina ya maziwa unayompa. Pale anapotapika au kuharisha hii inaweza kuwa shida ya mzio hivyo kuwasiliana na daktari ili upate suluhu.


Jinsi ya kutunza maziwa yako?

Siku zote usitunze maziwa yaliyobaki kwenye chupa. Unapochanganya maziwa hakikisha usichanganye maziwa mengi yatakayobaki. Weka kwenye jokofu maziwa yako yaliyo wazi na yatumike ndani ya masaa 48. Pia unapokuwa na maziwa ambayo tayari yamekwisha changanywa lakini hayajanyweka katika chupa, yaweke ndani ya jokofu na yatumie ndani ya masaa 24. Kama maziwa yako ya kanuni yamebaki kwa zaidi ya masaa 2 baada ya kunyweka, yamwage.


Tunza maziwa yako ya kukamua kwenye jokofu lako si zaidi ya siku 7 au yagandishe. Maziwa ya mama yanaweza kuhifadhika kwenye jokofu kwa miezi 3 katika joto la 18o C, au kwa miezi 6 kama ni kwenye friza.


Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org


Picha ni kwa hisani ya Dar 24.

62 views

Recent Posts

See All

Комментарии


bottom of page