top of page
C-Sema Team

Vitu gani vya kuzingatia wakati wa unyonyeshaji?

Updated: Aug 30, 2023

  • Mosi ni kuchunguza. Chunguza dalili za kuwa na njaa kwa mwanao na umnyonyeshe mwanao pale anapokuwa na njaa. Huu ndio unaoitwa unyonyeshaji pale palipo na uhitaji. Usisubiri mpaka mwano alie ndipo umnyonyeshe kwani wakati huo atakuwa na njaa kupita kiasi. Mama anatakiwa amnyonyeshe mwanae angalau mara 10 kwa siku au kila anapohitaji kunyonya.


Nitajuaje mtoto ana njaa? Mtoto anapokuwa ana njaa huwa ana ananyonya vidole vyake au huwa anapeleka vidole vyake kinywani mwake. Huwa anatoa sauti kama anayenyonya au hupiga miayo au kugeukageuka kuelekea ziwa.

  • Pili ni kuwa na subira. Usiwe na haraka wakati wa unapokuwa unamnyonyesha mwanao. Kuwa na subira na mnyonyeshe mwanao kadri anavyotaka walau mara 10 kwa siku.

  • Tatu na mwisho ni ‘kujinafasi’. Tulia unapokuwa unamyonyesha mwanao na maziwa yakutosha yatoka kwa ajili ya mwanao. Tafuta sehemu ambayo utaweza kukaa kwa kujinafasi. Unaweza kutafuta utulivu kwa kuegemeza shingo yako au miguu yako kabla ya kuanza kunyonyesha kama unapata shida.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org


2 views
bottom of page