top of page
  • C-Sema Team

Utaepukaje kifo cha ghafla cha mwanao?


Je, umewahi kusikia watoto wachanga wakifa usingizini ghafla tu? Kinga ni bora kuliko tiba. Kumbuka kuchukua tahadhari kila unapokuwa ukimlaza mwanao kitandani iwe mchana au usiku.


Hapa chini kuna mapendekezo ya kitaalamu kumwepusha mwanao na kifo cha ghafla: -


  • Unapomlaza mwanao mlaze kwenye sehemu ngumu isiyobonyea bonyea, mfano mzuri ni mkeka. Haishauriwi kutumia sofa, kiti au viti vya gari kama kitanda cha mwanao mara kwa mara.

  • Mara zote jitahidi kumlaza mwanao mchanga chali na si vinginevyo.

  • Jitahidi kadiri inayowezekana usilale kitanda kimoja na mwanao. Hii ni kwa sababu unaweza kusinzia ukajisahau na pasipo kukusudia ukamlali mtoto na kumsababishia madhara n ahata kifo cha ghafla.

  • Jitahidi ukiweza usimfunike miguo mingi mfano bebishoo, blanketi, mito, n.k. Hii ni kwa sababu anaweza kujiviringa katika miguo hiyo na kupata madaha n ahata kifo cha ghafla. Vilevile miguo hii inaweza kumsababishia joto kali asiloweza kulivumilia ikapelekea mauti ya ghafla.

  • Katika kutengeneza kitanda cha mwanao usiache nafasi kubwa ambayo mtoto anaweza kujiviringisha na kunyongwa.

  • Mwekee mwanao mpira wa mtoto (titibandia – pacifier) wakati wowote anapokuwa amelala kwani inaweza kumsaidia kupunguza hatari ya kupata ya kifo cha ghafla.

  • Hakikisha unapanga muda hasa wakati wa mchana kumlaza mwanao kwa kulalia tumbo ukimwangalia ili aweze kukomaa misuli yake ya shingo. Hii baadaye itamsaidia kuweza kukaa kwa urahisi muda ukifika. Haya ni mazoezi na siyo kumbembeleza asinzie. Hapa unamwandaa na si kumlaza. Ufanye kama mchezo huku ukimchekesha ili awe anainua shingo na kuifanyia mazoezi.

  • Kamwe usivute sigara ndani ya chumba cha mtoto.

  • Mwisho. Kumbuka kumnyonyesha mwanao kama inavyotakiwa. Soma Makala zetu juu ya unyonyeshaji www.sematanzania.org na ufuate maelekezo sahihi. Kamwe usijaribu kunyonyesha mtoto ukiwa umechoka kwani unaweza kusinzia na kumletea madhara kama kumuangusha ukiwa usingizini na kumsababishia madhara makubwa n ahata mauti.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org

0 views

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page