top of page
  • C-Sema Team

#SimuliziZa116: Mtoto wa miaka miwili apata matibabu


Mnamo 12 Mei 2018, mama Fadhili* (siyo jina lake halisi), mtoto mwenye umri wa miaka miwili alipiga simu namba 116 ya Huduma ya Simu kwa Mtoto akiwa nyumbani kwake kijijini Ushirombo wilaya ya Bukombe. Mama Fadhili aliripoti kwamba mwanae ametelekezwa na baba yake mzazi kwa kutotoa fedha za matumizi na matunzo muhimu kwa malezi ya mtoto. Mama Fadili alisema ni muda sasa hali yao si nzuri ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa henia uliokuwa unamsumbua mtoto Fadhili ukiachia mbali ukweli kwamba mara kadhaa mtoto alishinda na kulala njaa.


Mama Fadhili akaomba tumsaidie kupata ahueni.

Tuliwasiliana na Afisa Ustawi wa Jamii wa wilayani Bukombe amabaye aliandaa jalada na kumfikisha Baba Fadhili mahakamani kwa kesi ya kupuuza matunzo kwa mwanae. Siku ya Ijumaa tarehe 25 Mei 2018 mahakama iliamuru kuwa Baba Fadhili aanze mara moja kutoa matunzo kwa mtoto wake pamoja na kulipia gharama za matibabu ikiwamo operesheni ya hinia aliyotakiwa kufanyiwa mtoto wake.


Huduma ya Simu kwa Mtoto inapatikana kote nchini kwa kupiga simu namba 116 bila malipo na imewaunganisha maelfu ya wazazi wenye mahitaji kama Mama Fadhili kupata huduma stahiki kwa watoto wao. Tunawaasa wanajamii msikae kimya muonapo mtoto akipitia wakati mgumu.


Tupigie simu namba 116 tuzungumze!

0 views

Recent Posts

See All

Commentaires


bottom of page