top of page
C-Sema Team

Kujamiiana kwa mipango ili kupata mtoto.


Hapa kuna maswali yanayoulizwa mara kwa mara na wenzi wanaotafuta mtoto. Ni mara ngapi tunahitaji tujamiiane / kukutana? Jibu ni mara nyingi.


Wenzi wengi hutumia nguvu nyingi katika kuvizia muda ambapo yai linapokuwa linapevuka, wakitumia kanuni mbalimbali katika kukokotoa pale ambapo mwanamke anapokuwa tayari kwa ajili kupevusha mayai. Licha ya njia hii kinadharia kuonekana kuwa na mashiko. Tafiti za hivi karibuni zimeonesha kwamba kipindi cha mbegu kurutubisha yai ni kifupi. Na kwa kweli, ni siku 3-5 kuelekea kwenye upevushaji na siku ya upevushaji yenyewe.


Nafasi yako bora kabisa ya kuvizia yai kwa ajili ya urutubishwaji ni siku 1-2 kabla ya upevushaji. Hii ni kwa sababu yai baada ya kupevushwa yai la mwanamke huishi siku moja na lisipopevushwa hufa. Mbegu za mwanaume huishi mpaka masaa 48 kabla ya kufa. Madktari hupendekeza kujamiana kila baada ya siku moja ili kuongeza uwezekano wa kupata yai na kulilirutubisha. Hii ikiwa ni kipindi cha kuanzia kabla ya kuona siku na baada ya kuona siku.


Wakati ukijamiana na mwenzi wako katika siku hizo chache za kuvizia yai kupevuka kumbuka jambo lenye mantiki. Kumbuka kwamba kuna hasara zake- kwani kimsingi mwili wako huwa haufanyi kazi kwa kuzingatia kutimiza wakati (kalenda) kwani mwili huwa unathiliwa na vitu vingi ikiwemo mazingira nje ya mwili wako. Hata kama mzunguko wako na ule usio badirirka badirika hedhi inaweza kupatikana wakati wowote ule ndani ya mzunguko.


Kama unajamiiana kwenye siku unayodhani kwamba yai linapevushwa na hujamiiani kabla ya hapo au baada unaweza kujikuta uko kwenye bahati mbaya.


Hivyo, ili kulinda hizo bashiri zako fanya tendo la ndoa mara mbili au tatu kila wiki. Iwapo mwanaume ana kiwango kinachotakiwa cha mbengu, kujamiiana kila baada ya siku huongeza uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito.


Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org


1 view
bottom of page