top of page
  • C-Sema Team

Kuhusu uwezekano wa kupata ujazito.

Hili ni swali la msingi. Ni upi uwezekano wa mama kupata ujauzito ndani ya mwezi? Uwiano wa mwanamke kupata ujauzito ni asilimia 15% mpaka 20% katika mwezi wowote ule husika.Hivi hapa ni baadhi ya vitu vinavyoathiri uwezekano wako wa kupata ujauzito: -

Umri. Baada ya kuwa umefikia umri wa miaka 30 na zaidi, uwezekano wako wa kupata ujauzito katika mwezi wowote husika huwa unashuka. Na hushuka kwa kasi unapofikia umri wa miaka 40 au zaidi.


Mzunguko wa hedhi unao badilika badilika. Kuwa na mzunguko wa hedhi unaobadilika badilika hufanya iwe vigumu kukokotoa siku ambapo yai linapevuka na kutoka kwenye kijifuko cha mayai (ovary), na kwa sababu hiyo siyo rahisi kujua wakati muafaka wa kujamiana ili kutungisha mimba.


Mara ngapi uanafanya mapenzi (kujamiana). Kadri unavyofanya mapenzi mara chache ndivyo unavyopunguza uwezekano wa kupata ujauzito kwani hupunguza uwezekano wa kutungisha mimba. Lakini pia mwanaume anapofanya mapenzi mathalani kila siku hupunguza uwezekano wa kutungisha mimba kwani hataweza kutoa mbegu za kutosha na zilizo komaa zenye vigezo muhimu katika kutungisha mimba. Hii ni kwa sababu mbegu huzalishwa kila baada ya masaa 72.


Kiwango cha muda kilichotumia katika kutafuta ujauzito. Kama ujauzito haujapatikana katika kipindi cha mwaka mmoja au zaidi tangu wenzi walipoanza kutafuta mtoto, uwezekano wao wa kupata mtoto unaweza kuwa mdogo. Wenzi hao wawasiliane na daktari wao kuhusu kuwafanyia vipimo ili kuona kama kuna shida kwenye urutubishwaji.


Maradhi au dosari za kimaumbile zinaweza kuchangia uwezekano wa kupata ujauzito.


Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org


Picha ya makala ni kwa hisani ya Pregnancy.Org

24 views

Recent Posts

See All

Yorumlar


bottom of page