top of page
  • C-Sema Team

Fanya hivi kumsaidia mwanao kupata usingizi mwanana.

Pale unapomuona mwanao amelala kamwe hutaacha kutafakari uzuri wake na kumshukuru Mungu kwa uumbaji wake! Hata hivyo watoto wengi huwa na changamoto ya kulala au kupata usingizi.Punguza dukuduku na msongo wa mawazo kwa kuandaa vizuri ratiba ya usingizi ya mwanao kwa kuzingatia kile kinachowezekana na kile kisichowezekana katika ratiba.

Elewa mahitaji ya usingizi ya mwanao. Ni vizuri kujua kwamba katika miezi miwili ya kwanza baada ya kuzaliwa hitaji la kunyonya linakuwa juu ya hitaji lake la usingizi. Mara nyingi huwa ananyonya kila baada ya masaa 2.


Mtoto huwa hajui tofauti ya mchana na usiku. Hivyo huwa analala bila ya kujali ni wakati gani wa siku, mchana au usiku. Mtoto anaweza kulala kuanzia saa 8 mpaka 18 kwa siku lakini kwa vipande vya 3 mpka 4 kisha huamka. Wengi wa watoto wanapofikia muda wa miezi 3 mpaka 6 huwa wana uwezo wa kulala kwa masaa 6 mfululizo. Anapofikia miezi 6 mpaka 9 kutokana na mabadiliko ya ukuaji anaweza kubadili ratiba yake. Hapo anaanza kuhisi upweke unapokuwa mbali naye na huwa analia ili uwepo pale kumuondolea upweke.


Weka ratiba ya kwenda kulala. Baadhi ya wazazi huwa wanawatengenezea watoto wao utaratibu wa kwenda kulala mapema kuanzia wiki 6 mpaka 8 kila mchana. Ratiba ya mwanao inaweza kutokana na muunganiko wa shughuli zinzaofanya wakati wa kulala. Mambo haya yanaweza kuwa msaada wako katika kumsaidia mwanao kulala: -

  • Watoto wengi wanafurahia kuoga kabla ya kwenda kulala kwani kitendo hili kinawapatia utulivu.

  • Weka ratiba ya michezo ya mtoto wako kila siku usiku katika mpangilio ule ule.

  • Mchezeshe mwanao michezo yenye shughuli nyingi mchana na shughuli chache wakati wa usiku. Hii itamsaidia mwanao asichangamke sana wakati wa usiku kwani anahitaji utulivu kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya kulala na anahitaji uchangamfu mchana ili kujifunza.

  • Shughuli zake wakati wa usiku ziwe tulivu na chache zikipungua kadri muda unvyokwenda.

  • Fanya mazingira ya chumbani kuwa yasiyo badilika. Taa na sauti ndani ya chuma zisibadilike wakati wa usiku wa manane ili asishituke na kuamka wakati wa usiku.

  • Mchezo aupendao mwanao uwe wa mwisho wakati wa usiku. Hii itamsaidia kuwa na mshawasha wenye shauku kwenda chumbani na atauhusisha usingizi na vitu anavyovipenda.

Muweke mwanao aliye na usingizi kitandani. Mwanao napokaribia kulala muweke kitandani. Mlaze kitandani na umwache alale mtindo anaoupenda. Usisubiri mpaka mwanao akala mikononi mwako kwani atakapozoea itakuwa ngumu kuirekebisha tabia hii hapo baadae. Anza kumbembeleza mwanao mpaka atakapolala kuanzia wiki 6 mpaka 12.


Utaratibu huu utamfundisha mwanao kujibembeleza mwenyewe ili kulala. Hutakuwa na haja ya kumbembeleza na kumhamasisha kulala kila anapoamka usiku toka usingizini.


Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org


Picha ni kwa hisani ya UNICEF

2 views

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page