Ufahamu juu ya mzunguko wa hedhi husaidia. Mzunguko wa hedhi huanza siku ya kwanza pale ambapo mwanamke anapoona damu nyekundu na siyo tu matone. Mzunguko huisha siku moja kabla mzunguko mwinge haujaanza. Mzunguko wa hedhi unaweza kuanzia siku 21 mpaka 35 au zaidi.
Iwapo urefu wa mzunguko wa hedhi unatofatiana mwezi huu na mwezi mwingine kwa siku kadhaa, mzunguko huo huchukuliwa kuwa ni mzunguko unaobadilika badilika. Hii ni kawaida kwani wanawake wengi huwa hawana mzunguko usio badilika badilika. Hii haimaanishi kuwa wana tatizo. La hasha! Wako salama kabisa.
Kikokotoo cha urutubishwaji yai kipo matengenezoni. Tutakiweka hapa hivi punde. Asante kwa kutuelewa!
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org
Comments