top of page
  • C-Sema Team

Afya ya kinywa kwa mtoto.


Kwa kawaida, mtoto huanza kuota meno kuanzia miezi 6-12 japo inaweza kuwa awali ya hapo. Jino la kwanza linapojitokeza, ni vyema mzazi uanze kumsafisha mtoto kinywa maana huo ndio wakati sahihi. Soma zaidi kufahamu namna ya kusafisha kinywa cha mwanao na namna ya kumsaidia ajifunze usafi wa kinywa anavyozidi kukua.


Miezi ya mwanzo kuanzia miezi 6-12, ni vyema mzazi utumie kitambaa kisafi na laini chenye dawa ya meno kiasi sawa na punje ya mchele. Safisha meno ya mtoto taratibu. Kitambaa ni salama maana ni laini hivyo hakitamuumiza fizi.


Inashauriwa mtoto aswaki angalau mara mbili kwa siku (vivyo hivyo kwa watu wazima) – yaani asubuhi akiamka, na baada ya mlo wa mwisho jioni kabla hajalala. Mtoto asukutue baada ya kila mlo ili kuondoa masalia ya vyakula yanayoleta harufu mbaya na vijidudu mdomoni.


Mwanao anavyokua mfundishe kuswaki meno vizuri huku akisafisha fizi na ulimi pia. Ni wajibu wako kama mzazi kumfundisha mtoto wako namna ya kusafisha meno yake kwa usahihi. Jitahidi kuhakikisha unabadili mswaki wa mwanao kila baada ya miezi 3-4, ama mtoto anapoumwa na pale mswaki unapoanza kuchambuka.


KUMBUKA: Kwa usalama zaidi, inabidi kuzingatia kuwa mtoto anakula mlo kamili; epuka vyakula vyenye sukari ili uepuke meno yake kuoza. Tumia dawa yenye floridi (fluoride) na mtoto ajifunze kutema dawa kabla ya kusukutua na maji.

1 view

Recent Posts

See All
bottom of page