top of page
  • C-Sema Team

#SimuliziZa116: Watoto wawili yatima wapata mlezi kwa uasili (adoption)


Ilikuwa ni siku tulivu ambapo mshauri wetu katika kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto #116 alipokea simu ya Bwana Juma Said aliyepiga kutoka kijiji cha Buharangwa mkoani Kigoma. Bwana Saidi alisema kwamba anahitaji kupata kibali ili aweze kuwalea watoto wa marehemu kaka yake ambao ni Twaha mwenye umri wa miaka 9 na Amina mwenye umri wa miaka 7. Bwana Saidi aliendelea kusema hivi sasa Twaha na Amina wemepoteza wazazi wao wote wawili na wanaishi kwa babu yao ambaye pia ni mzee sana na anasumbuliwa na ugonjwa wa ukoma hivyo kushindwa kupata mahitaji muhimu.


Mshauri wetu alianza kushughulikia kibali cha Bwana Said kwa kufanya mawasiliano na Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya na kumueleza juu ya ombi la Bwana Saidi la kutaka kupata kibali cha kuwalea watoto wa marehemu kaka yake. Afisa ustawi alimpa Bwana Saidi maelekezo ya kufuata ili kuweza kupata kibali.


Kwa kuwa Bwana Saidi ni mwana familia alihitaji kupata kibali cha uasili wa wazi ambapo alihitaji kupata uthibitisho wa serikali ya mtaa na pia kujaza fomu maalumu ya uthibitisho wake kama raia wa Tanzania. Vilevile alipaswa kuthibitisha kuwa ataweza kuwalea watoto vizuri na kuwapatia mahitaji muhimu. Mwisho aliombwa kuambatanisha vielelezo kama hati ya nyumba, barua ya mwajiri na wadhamini ili kumthibitishia uwezo wa kumudu jukumu la malezi.


Hata hivvo wakati zoezi la kupata kibali cha kudumu likiendelea (uasili) aliruhusiwa kuwachukua watoto na kukaa nao kwa muda wa miezi sita akiwa chini ya uangalizi wa Ofisi ya Ustawi wa Jamii ili kuthibitisha kuwa anao uwezo wa kuwahudumia watoto vizuri. Bwana Saidi alifanikiwa kupata viambatanisho vyote na uthibitisho wa kuwa ataweza kuwalea watoto vizuri hivyo kupatiwa rasmi kibali na kuanza kuwalea watoto.


Twaha na Amina walifanikiwa kuhama walipokua wakisoma awali na kujiunga na shule nyingine wakiwa makao katika makao mapya. Hivi sasa wanafurahia maisha mapya na wanahudhuria masomo kama watoto wengine.

Simu ya huduma ya mtoto#116 inaendelea kusikiliza na kufikia watoto wengi zaidi hata sasa.


Tafadhali piga namba #116 sasa uzijue huduma za mtoto hapa Tanzania ama uweze kushiriki kumuokoa mtoto aliye katika mazingira magumu. Mwambie rafiki tufanye jamii kuwa bora zaidi kwa malezi ya watoto wetu. Inawezekana. #SimuliziZa116 #Malezi

1 view

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page