Kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto kilipokea simu kutoka baba mmoja ambaye aliripoti kwamba mke wake amebakwa. Mhalifu ambaye alikuwa akiendesha gari alipaki na kuomba kujisaidia nyumbani kwao na baada ya kumaliza haja yake alipata kusikia mazungumzo ya mke na mume kuhusu kwenda sokoni na akapendekeza kumpa mke lifti kwani alikuwa anaelekea njia hiyohiyo.
Njiani alimuomba mama mwenye nyumba namba ya simu na wakakubaliana atampa lifti ya kurudi nyumbani baada ya manunuzi sokoni. Kama alivyoahidi mama huyu alimpigia simu naye alimpa tena lifti kurudi. Mara hii alibadilisha njia na alipoulizwa mbona njia nyingine dereva aling'aka pasi kutoa majibu.
Mama yule alizirai na alipozinduka alikuwa tayari keshabakwa na kuachwa njiani. Alimsimulia mumewe kisa hiki na wakaelea polisi ambako mtuhumiwa aliitwa na kukiri kosa. Aliwataka mume na mke wakubali fidia ambayo mume aliikataa kwa hasira. Hapo ndipo Baba huyu (mume) alipoamua kutupigia simu.
Alitueleza kuwa ametoa taarifa hadi kwa Mkuu wa Wilaya pasi ufunguzi. Alitueleza yuko tayari hata kuingia gharama za safari hadi Unguja ikiwezekana kumuona raisi wa Zanzibar.
Tuliipeleka kesi hii kwa Idara ya Wanawake na Watoto Mwanakwerekwe (Makao Makuu) ambao waliwasiliana na Mamlaka za Serikali Pemba na kufanikiwa kuipeleka kesi hii mahakamani. Bahati mbaya mke-mtu alikataa kubakwa mbele ya hakimu / mahakama na hivyo kesi ikafutwa. Mume na mke wameachana toka wakati huo.
Huduma ya Simu kwa Mtoto hupatikana mitandao yote Zanzibar na Tanzania Bara pasi malipo kuwahudumia watoto na mara chache akina mama. Tupigie 116 kutoa taarifa za ukatili dhidi ya akina mama na watoto.
Yorumlar