top of page
  • C-Sema Team

#SimuliziZa116: Baba apandishwa kizimbani kwa ukatili wa kingono kwa mwanae.

Tarehe 7 Disemba 2017 tulipokea simu kutoka kwa mama aliyeongea kwa uchungu mkubwa. Alijitambulisha kama mama Mariam mkazi wa wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam. Alitueleza kuwa aliyekua mumewe ambaye ni baba wa Mariam alimtorosha mtoto wao kwenda mkoani Songea bila idhini yake.Mama huyo alieleza kuwa alipigiwa simu na mama wa kambo wa Mariam akieleza kutoridhishwa na mwenendo wa baba mtu kwa bintiye. Alielezwa kuwa baba Mariaum alikuwa akimuingiza vidole sehemu za siri mtoto Maria mwenye umri wa miaka mitano (5). Kwamba alifanya hivi kwa kisingizio cha kumuogesha na hata alivyoulizwa aling'aka na kutoa maelekezo kwamba ni yeye tu ndiye atakeye endelea kumuogesha binti yake. Tukio hili lilimhuzunisha sana mama Mariam naye akatupigia.


Tulizungumza na Afisa Ustawi wa Jamii na kwa kushirikia na Dawati la Jinsia na Watoto - Polisi Manispaa ya Songea waliamua kufunga safari kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa baba Mariam kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Walijiridhisha kuwa taarifa hizo ni za kweli na kuamua kumpeleka mtoto hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Huko ilibainika kwamba mtoto Mariam ameingizwa vidole sehemu za uke na alipatiwa matibabu.


Mariam alibaki kwa Afisa Ustawi Songea wakati taratibu za kuunganishwa na mama yake zikiendelea. Baba Mariamu alifunguliwa mashtaka ya kummnyanyasa mtoto wake kingono, Kituo Kidogo cha Polisi Misufini. Mnamo tarehe 18 Disemba 2017 shauri lake lilisikilizwa kwa mara ya kwanza na alikutwa na hatia ya kumfanyia mtoto wake vitendo vya kikatili.


Sheria ya Mtoto inatamka wazi kwamba mtu hataruhusiwa kumsababishia mtoto mateso, au aina nyingine ya ukatili au kumdhalilisha mtoto ikijumuisha mila na desturi zozote zenye madhara kwa mtoto kimwili. Tupigie simu namba 116 tuzungumze. Kukaa kimya ni kushiriki uovu.

1 view

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page