
Kisa hiki kimetokea mwaka jana wakati wa sherehe za Idd mjini Unguja. Binti mwenye ulemavu wa akili aliachwa nyumbani, kote kumefungwa huku ndugu na wazazi wake wakienda sherehekea Idd majira ya jioni (usiku wa mapema). Bahati mbaya dirisha la chumba alimokua amelala lilivunjwa na walifanikiwa kumbaka na kumlawiti hata mauti.
Yaani mtoto mwenye ulemavu wa akili alibakwa na kama haitoshi kulawitiwa mpaka kifo tena siku ya Idd. Daktari (Pathologist) toka kituo cha huduma ya afya Mnazi Mmoja Unguja alidhibitisha kifo kilitokana na kubakwa huku amebanwa pua na mdomo kwa nguvu hadi hewa na pumzi zikamtoka na kupelekea kifo cha binti huyo.
Bahati mbaya hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hili hadi leo. Funzo hapa ni kwamba iwapo tunapanga kutoka nyumbani, tutoke na watoto wote asiachwe nyuma hata mmoja na iwapo itabidi kuachwa basi pawepo na uangalizi wa watoto wetu sherehe hizi za Idd.
Eid Mubarak toka Ugunja!