top of page
  • Writer's pictureIzabel Simiyu

Maria Apata Msaada

Updated: Jun 9, 2023

Mwezi uliopita, Maria binti wa miaka 11 alimweleza mwalimu wake (Mwalimu Joshua) kuwa baba yake amembaka. Japo Mwalimu Joshua alishtushwa na habari hii aliendelea kumsikiliza Maria kwa umakini.


Maria aliendelea kufunguka na kumwambia mwalimu kuwa ameishi na baba yake baada ya yeye na mama yake kutengana na baba huyo alikua akimnyanyasa mara kwa mara na hatimaye kumbaka, hakujua afanye nini na nani atamsaidia.


Mwalimu Joshua alimfariji binti huyu na kumwahidi kulifanyia kazi na kumsaidia.

Bila kupoteza mda alitupigia 116 na kutupa taarifa hii, mtoa huduma wetu aliipokea kesi na kuipeleka moja kwa moja kwa Afisa Ustawi.


Afisa alikwenda polisi kupata PF3 itakayomsaidia Maria kupata matibabu na baba yake alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Kwa sasa Maria anaendelea vizuri anaishi na mama yake na baba amehukumiwa miaka 30 jela.


Inahuzunisha sana kwamba kesi kama hizi bado zinatokea, mzazi unatakiwa kuwa mtetezi na mlinzi wa kwanza wa mtoto wako na sio mtuhumiwa. Itufikirishe!


9 views

Comments


bottom of page