top of page
  • C-Sema Team

#116Stories: Adhabu kali za viboko haziwajengi watoto wetu!

Mwezi uliopita, Amani (sio jina lake halisi) mtoto wa miaka 11, alipiga simu 116 akiitaji msaada juu ya adhabu kali ya viboko wanazopewa shuleni kwao. Amani alitueleza kuwa, mwalimu wake mmoja huwachapa wanafunzi sana sehemu yoyote ya mwili mara nyingi bila kusikiliza maelezo yao.


Kuna siku Amani alisahau daftari lake la shule nyumbani, mwalimu alivyofanya ukaguzi na kugundua kuwa hana daftari hilo alimpeleka mbele ya darasa na kumchapa sana.


Amani alivyorudi nyumbani aliwaambia wazazi wake na pamoja walikwenda shule pamoja kuzungumza na uongozi wa shule ambao walikubali kulishugulikia. Ila baada ya wiki kadhaa Amani hakuona tabia ya mwalimu kubadilika ndipo alipopiga Huduma ya Simu kwa Mtoto.Siku hiyo hiyo tulipeleka kesi hiyo kwa Afisa Ustawi (SWO) aliyekuwa karibu nao. SWO na VEO waliitisha kikao na Amani, wazazi na walimu wake. Waligundua kwamba mwalimu mkuu hakuwa amechukua hatua yoyote juu ya malalamiko yaliyotolewa na sio mara ya kwanza.


Walikubali kuwa na kikao shuleni na walimu wote. Kwa kuwa haikuwa mara ya kwanza kwa mwalimu huyo kufanya kitu kama hicho bila kuchukuliwa hatua yoyote, waliamua kumpa adhabu ya kusimamishwa kazi kwa mwezi 1 bila malipo kama athari ya matendo yake.

Pia, walielezwa jinsi adhabu kali zinavyowaathiri watoto na kutishia usalama wao. Walipanga kuwa na vikao vya mara kwa mara kujifunza namna gani wataweza kuwaadabisha watoto bila adhabu hizo.


Kwa maswali au ushauri piga 116 Huduma ya Simu kwa Mtoto.


2 views

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page