top of page
C-Sema Team

#116Stories: Vyakula vya ziada kwa kumpa mtoto wa miezi tisa.

Mnamo tarehe 31 Desemba, baba Adam alitupigia simu akitafuta ushauri juu ya vyakula gani amlishe mtoto wake wa miezi 9. Alitueleza kuwa, kwa mda ule walikua wakimnyonyesha na kumpa uji kama chakula cha ziada.



Mshauri wa huduma ya simu kwa mtoto alimwelekeza baba Adam juu ya vyakula bora vinavyopendekezwa na wataalamu wa lishe ya mtoto, kama nyama na samaki laini, wali, ugali mlaini, matunda kama maembe na machungwa ambayo pia yanaweza kutengenezwa kuwa juisi laini na bila kusahau mboga mboga kama spinach na mchicha.


Vyakula hivi vyote vikiambatanishwa na maziwa ya mama vinaweza kumpa mtoto virutubisho anavyoitaji katika ukuaji wake na kuifanya afya yake iwe imara. Mshauri alimsisitiza baba Adam azingatie sanasana vyakula hivyo vitengenezwe kwa hali ya usafi na viwe vilaini ili mtoto aweze kumeza vizuri.


Baba Adam alishukuru kwa ushauri aliopewa na aliahidi kutupigia tena japo atakua na maswali mengine ya ziada.


Kwa maoni na ushauri wasiliana nasi kupitia namba 116, Huduma ya simu kwa mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo yoyote. #Malezi #SimuliziZa116 #116Stories

112 views
bottom of page