Last updated 2 years ago
Kumbuka dondoo hizi unapolazimika kumhudumia mjamzito wakati wa kujifungua:
Kila unapokuwa na mjamzito fanya maandalizi yote ya wepesi wa kumfikisha hospitali. Kujifungulia mtoto hospitali ni salama zaidi ya kujifungulia nyumbani.
Hizi ni dalili za hatari wakati wa ujauzito.
Uchungu wa uzazi unaochukua muda mrefu sana. Uchungu wa uzazi wa zaidi wa saa 12 kwa mama aliyerudia kuzaa (mzoefu), au uchungu zaidi ya saa 24 kwa mama anayejifungua kwa mara ya kwanza ni hatari. Uchungu namna hii mara nyingi husababisha majeraha kwa mama na unaweza kuleta madhara kwa mtoto. Vilevile pale ambapo maji ya uzazi yataanza kutoka lakini uchungu wa uzazi ukawa umekawia kwa hadi saa 12 hii inaweza kusababisha maambukizi.
Shinikizo la juu la damu. Shinikizo la damu la 160/110 au zaidi ni dharura na hatari. Tafuta msaada wa daktari haraka na jiandae kwa ajili uwezekano wa kukumbwa ba kifafa cha mimba wakati wowote.
Homa. Unapopata homa au kusikia mapigo ya moyo wa mtoto yanakwenda haraka, huenda kuna maambukizi kwenye tumbo la uzazi ambayo yanaweza kumuathiri mama na mtoto. Tafuta msaada wa daktari.
Mtoto aliyelalia upande katikati ya njia ya uzazi (bila kukaa wima). Huu ni mkao ambao hauwezi kuruhusu mtoto kuzaliwa kwa njia ya kawaida. Operesheni hospitalini inahitajika mara moja ili kunusuru maisha ya mtoto. Mama apelekwe hospitalini haraka.
Kiunga mwana (placenta) kinapotoka nje kabla ya mtoto kuzaliwa. Tukio hili hutokea kwa nadra na linaweza kusababisha kichwa cha mtoto kugandamiza kiunga mwana na kutoruhusu damu kumfikia mtoto. Mtoto atanusurika tu kama mama atawahishwa hospitalini kwa ajili ya operesheni. Mama anapaswa kubaki akiwa amejiegemeza kwenye mikono na magoti yake sehemu ya kiunoni ikiwa imeinuliwa juu kupunguza mgandamizo kwenye kiunga mwana.
Vifaa na mahitaji kwa ajili kujifungua.
Kwa ajili ya kujifungua salama, andaa vifaa vifuatavyo: -
Muhimu – Unapokwenda kliniki jitahidi kuuliza mahitaji muhimu na vifaa vya kuandaa kwa ajili ya kujifungua. Watakueleza vyema ili ujipange kuepusha purukushani siku ya siku.
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania, Instagram @sematanzania na www.sematanzania.org